Majukumu ya TFDA

MAJUKUMU YA
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA)
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Semina Elekezi WAUJ, AICC Arusha
2 - 6 Octoba 2006
Margareth Ndomondo-Sigonda
Mkurugenzi Mkuu - TFDA
1
www.tfda.or.tz
Yaliyomo
•
•
•
•
•
•
•
•
Utangulizi
Majukumu ya TFDA
Muundo wa TFDA
Wadau wa Mamlaka
Mafanikio
Changamoto
Matarajio
Hitimisho
2
www.tfda.or.tz
Utangulizi
• Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyoko chini ya
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayosimamia udhibiti wa ubora
na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
• TFDA imepewa madaraka ya kufanya maamuzi mbalimbali ya
kiutendaji kwa mujibu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya
mwaka 2003 na ile ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997
• Mamlaka ilianza kutekeleza majukumu yake rasmi tarehe 1 Julai
2003
• Dira ya TFDA ni kuwa taasisi bora katika udhibiti wa ubora na
usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kwa nchi za Afrika
ifikapo mwaka 2015
• Lengo la Mamlaka ni kulinda afya ya wananchi na jamii yote kwa
ujumla kwa kuzuia madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana
na matumizi ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
3
www.tfda.or.tz
Majukumu ya TFDA
• Kutathmini na kusajili vyakula, dawa, vipodozi na vifaa
tiba
• Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa kwa kudbibiti
utengenezaji, uingizaji na usambazaji wa vyakula, dawa,
vipodozi na vifaa tiba
• Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakikisha kuwa
bidhaa husika zinafikia viwango vya ubora na usalama
• Kusimamia majaribio ya dawa mpya na vifaa tiba
(Clinical trials)
• Kutoa leseni na vibali mbalimbali vya kuendeshea
biashara ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
• Kudhibiti utoaji wa matangazo ya biashara ya bidhaa
zinazodhibitiwa na TFDA
• Kuratibu madhara yatokanayo na utumiaji wa vyakula,
dawa, vipodozi na vifaa tiba
• Kuelimisha jamii kuhusu ubora, usalama na matumizi
sahihi ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
4
www.tfda.or.tz
Muundo wa TFDA
•
Ofisi ya Mkurugenzi mkuu
– inayo Maafisa wanaoshughulikia masuala ya sheria, uhakiki
wa mifumo, uratibu wa ofisi za kanda na serikali za mitaa,
Mpango wa maduka ya Dawa Muhimu na uhusiano
•
Kurugenzi ya Uendeshaji Huduma
–
•
husimamia utawala, fedha, elimu kwa umma, na kuhakikisha
kwamba shughuli mbali mbali za Mamlaka zinafanyika kwa
ufanisi
Kurugenzi ya Tathmini na Usajili wa Bidhaa
–
hutathmini taarifa mbalimbali za chakula, dawa, dawa za
mitishamba, vipodozi, na vifaa tiba kabla ya kuidhinishwa
kwa matumizi
5
www.tfda.or.tz
Muundo wa TFDA (2)
• Kurugenzi ya Ukaguzi na Ufuatiliaji
– hufuatilia na kuchunguza usalama wa vyakula, dawa,
dawa za mitishamba, vipodozi na vifaa tiba. Pia
hukagua sehemu zote zinazojihusisha na biashara za
bidhaa hizi ili kuhakikisha kama taratibu zinafuatwa
• Kurugenzi ya Huduma za Maabara
– hupima ubora wa vyakula, dawa, dawa za
mitishamba, vipodozi na vifaa tiba
6
www.tfda.or.tz
MINISTER MoH &SW
MINISTERIAL ADVISORY
BOARD
PERMANENT
SECRETARY MoH
DIRECTOR GENERAL
ADDO PROGRAMME
ZONE & LOCAL GOVERNMENT
COORDINATION
PUBLIC RELTAIONS
DIRECTORATE OF
BUSINESS SUPPORT
DIRECTORATE OF
INSPECTION AND
SURVEILLANCE
FINANCE
QUALITY ASSURANCE
LEGAL COUNSEL
DIRECTORATE OF PRODUCT
EVALUATION & REGISTRATION
DIRECTORATE OF
LABORATORY SERVICES
FOOD REGISTRATION
FOOD INSPECTION
CHEMISTRY
DRUG REGISTRATION
ADMINISTRATION AND
PERSONNEL
DRUG, COSMETICS
AND MEDICAL
DEVICES INSPECTION
MICROBIOLOGY
COSMETICS EVALUATION
PLANNING
REGISTRATION OF
PREMISES &
LICENSING
PUBLIC EDUCATION,
PHARMACOGNOSY
MEDICAL DEVICES
EVALUATION
REREGGREREGISTRATION
R
TECHNICAL SUPPORT
MANAGEMENT
INFORMATION SYSTEM
PRODUCT RISK ANALYSIS &
PROMOTION CONTROL
7
www.tfda.or.tz
Wadau wa Mamlaka
–
–
–
–
–
–
–
–
–
–
Wizara na idara mbalimbali za serikali k.m TBS,
Mkemia Mkuu wa Serikali, TAMISEMI na TPRI
Mashirika ya kimataifa k.m WHO, FAO, Codex
Alimentarius, UNICEF
Mashirika yasiyo ya kiserikali k.m MSH
Watengenezaji, waingizaji nchini, wasambazaji na
wauzaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
Wasimamiaji wa sheria
Wafanyakazi wa sekta ya Afya na watafiti
Vyombo vya habari
Vyama vya wafanyabiashara wa bidhaa
zinazodhibitiwa na Mamlaka
Watoa huduma mbalimbali
Walaji, watumiaji na wananchi wote kwa ujumla
8
www.tfda.or.tz
Mafanikio
• Uanzishwaji wa Mpango wa Maduka ya Dawa Muhimu (ADDO)
– Maduka 162 yamefunguliwa Ruvuma; 44 Wilaya ya Ulanga na 51
Kilombero (Morogoro). Uhamishaji na utambuzi wa Maduka ya Dawa
Baridi katika mikoa ya Mtwara na Rukwa umeshafanyika.
• Uanzishwaji wa mpango wa kuhakiki ubora wa dawa (QA
program)
– Maabara ndogo (Minilab kits) 10 za kuchunguza dawa zimewekwa
katika vituo vya mipakani na pia Mikoa ya Tanga, Mwanza, Ruvuma,
Mtwara, Mara, Kigoma na Dodoma
– Aidha simu za upepo (radio calls) zimefungwa katika vituo vya
Tunduma, Sirari, Horohoro na Namanga
• Mkakati wa kukuza viwango vya utengenezaji wa dawa nchini
– Ili viwanda viweze kukidhi masharti ya utengenezajo bora wa dawa
– Kuongeza upatikanaji wa dawa ambapo kwa sasa ~30% ya mahitaji ya
dawa nchini huchangiwa na viwanda vya ndani
– Kuweza kuuza nchi za nje na hivyo kuchangia uchumi wa nchi
9
www.tfda.or.tz
Mafanikio (2)
•
Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Client Service
charter)
–
–
•
Umetayarishwa na kuzinduliwa rasmi Januari 27, 2006
Mkataba huu unaainisha viwango vya utoaji huduma kwa wateja
k.m kutoa majibu ya uchunguzi wa maabara katika kipindi cha
siku 14, kutoa vibali vya kuingiza bidhaa katika kipindi cha saa
48, kushughulikia maombi ya leseni na usajili wa majengo katika
kipindi cha siku 45
Mkakati wa kukuza viwango vya utengenezaji wa
viwanda vya kusindika vyakula
–
–
Tathmini (baseline survey) ya viwanda vya kusindika vyakula
nchini ikiwa ni pamoja na wasindikaji wadogo wadogo
imefanyika
Lengo hasa ni kuendeleza sekta hii kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali
10
www.tfda.or.tz
Tathmini ya viwanda vya kusindika vyakula nchini
700
600
500
400
300
200
100
0
Total of No.of prem ises
Total
large
m edium
sm all
Micro
614
67
92
176
279
11
www.tfda.or.tz
Mafanikio (3)
• Uelimishaji wa wadau
– Semina za uelimishaji wa wadau kuhusu majukumu ya
TFDA zimefanyika nchi nzima ambapo jumla ya wadau
2500 wameshiriki
– Vipindi mbalimbali vya uelimishaji kwa njia ya radio,
televisheni na magazeti vimekuwa vikitolewa
– Vipeperushi mbalimbali na mabango (brochures, fliers &
banners) vimechapishwa na kugawanywa kwa wadau
kupitia mikutano, semina na maonesho (exhibitions)
– Mawasiliano yameimarishwa kati ya TFDA, wadau wake
na jamii kwa ujumla kwa kuanzisha Tovuti ya Mamlaka
ya Chakula na Dawa yaani www.tfda.or.tz
12
www.tfda.or.tz
Mafanikio (4)
• Ukaguzi
– Udhibiti wa ubora na usalama wa bidhaa umeimarishwa kwa kufanya
ukaguzi wa mara kwa mara katika;
• Viwanda vya kutengeneza dawa (ndani na nje) na vya kusindika vyakula
• Majengo ya biashara (maduka ya dawa, hoteli, supermarkets)
• Maduka ya Dawa Baridi k.m kati ya Mei na Agosti, 2006 maduka ya
dawa baridi 1,027 yalikaguliwa
– Dawa moto za thamani ya shilingi milioni 250 zilikamatwa
– Maduka 275 ya vipodozi yalikaguliwa na vipodozi vyenye viambato
vyenye sumu vya thamani ya shilingi milioni 27 vilikamatwa
– Jumla ya wakuguzi 707 wameshateuliwa kwa mujibu wa Sheria ya
Chakula, Dawa na Vipodozi (Makao Makuu, TAMISEMI, Vituo vya
Forodha) na wakuguzi 419 wameshapewa mafunzo
– Wakaguzi wametawanywa kwenye vituo vya Forodha vya Namanga,
Sirari, Tunduma, Kasumulu, Isaka, Horohoro, KIA, DIA, Tarakea,
Holili, Bandari Mwanza, Bandari Tanga na Bandari DSM
13
www.tfda.or.tz
Ukaguzi wa viwanda vya dawa (GMP) nje ya nchi
(2003-2006)
Mwaka
Idadi
iliyokaguliwa
Idadi
iliyofikia
cGMP
Idadi
isiyofikia
cGMP
% isiyofikia
cGMP
2003/04
35
26
9
25.71
2004/05
54
33
21
38.89
2005/06
45
30
15
33.33
14
www.tfda.or.tz
Ukaguzi wa viwanda vya dawa 2005/06
30
20
No of
prem ises
inspected
10
0
Tanzan
Russia
ia
Middle
East Bangla
desh
and
India
South
Malawi
Africa
Kenya
Far
Total
7
1
4
2
22
7
1
8
Com plied
4
0
4
1
14
5
0
6
Not cm plied
3
1
0
1
8
2
1
2
15
www.tfda.or.tz
Sampuli za dawa zilizochukuliwa wakati wa
ukaguzi (PMS) [2003 – June 2006]
Mwaka
Idadi
Iliyochukuliwa
katika soko
Idadi
Iliyochunguzwa
Idadi
Ilifaulu
Idadi
Iliyofeli
% Iliyofeli
2003
127
125
113
9
7.2
2004
183
167
142
25
14.97
2005/06
785
676 (517 643
(screening
+ 157 full
analysis)
33
4.9
16
www.tfda.or.tz
Mafanikio (5)
• Uanzishaji wa Mifumo Bora ya Utendaji kazi
(Quality Management)
– Maabara iko katika hatua nzuri ya utekelezaji wa
mfumo wa ISO 71025 (Laboratory accreditation
based on ISO 17025 standard)
– Mamlaka kwa ujumla wake imeanza kutayarisha na
kutekeleza mfumo wa ISO 9001:2000 (Quality
Management System based on ISO 9001:2000
standard)
– Lengo la TFDA ni kufikia viwango hivyo vya ubora wa
utendaji kazi ifikapo Juni 2008
17
www.tfda.or.tz
Mafanikio (6)
• Usajili wa bidhaa na uchunguzi wa kimaabara
– Usajili
• Jumla ya dawa 4087 (3685 za binadamu, 396 za mifungo na
6 za mitishamba) zimesajiliwa kati ya mwaka 1999 na Juni
2006
• Jumla ya vyakula vilivyofungashwa 3832 vimetambuliwa
(notified) na 213 vimesajiliwa (155 vya ndani, 34 vya nje ya
nchi na 24 ni vyakula dawa)
– Uchunguzi
• Mwaka 2001 wakati mpango wa QA unaanza sampuli
zilizofeli zilikuwa 13%
• Mwaka 2004/05 sampuli zilizofeli ni 3.7% (n= 1257)
• Mwaka 2005/06 zilikuwa 3% (n=1341) kwa sampuli zote za
dawa zilizochunguzwa
18
www.tfda.or.tz
Changamoto
•
•
•
•
•
•
•
Mabadiliko ya haraka ya teknologia, utandawazi na soko huria
unaosababisha ongezeko la bidhaa katika soko hivyo kuongeza
ugumu wa udhibiti
Uhaba wa raslimali ikiwa ni pamoja na fedha
Uwezo wa kuajiri watumishi wenye sifa na kuwapa motisha
Kusogeza huduma karibu na wanachi kwa kuanzisha na kuendesha
ofisi za Kanda
Kuweza kufikia viwango vya kimataifa vya ubora wa utendaji kazi
yaani ISO 17025 (Maabara) na ISO 9001:2000 (Mamlaka) ifikapo
mwaka 2008
Kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu na wadau
wasiofuata masharti ya sheria kwa hiari
Ongezeko la magonjwa mapya yasiyotibika
19
www.tfda.or.tz
Matarajio
•
•
•
•
•
•
Kuwepo chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba vyenye ubora
na usalama unaokubalika katika soko la Tanzania
Wananchi kuwa na elimu na taarifa mbalimbali kuhusu
chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
Kuanzisha ofisi za Kanda kwa lengo la kupeleka huduma
karibu na wananchi
Kueneza Mpango wa Maduka ya Dawa Muhimu (ADDO)
nchi nzima ifikapo mwaka 2012
Viwanda vya dawa na chakula vya hapa nchini kufikia
viwango vya utengenezaji bora kwa kuwapa mafunzo ya
GMP na HACCP wazalishaji
Kufikia viwango vya ubora vya utendaji kazi vya kimataifa
kwa maabara (ISO 17025) na TFDA kwa ujumla (ISO
9001:2000)
20
www.tfda.or.tz
Hitimisho
• Ili kuweza kutekeleza kazi na majukumu yake
kwa ufanisi, TFDA inahitaji ushirikiano kutoka
kwa wadau wake;
– Sekta ya Afya kwa ujumla wake
– TAMISEMI
– Wizara ya Mifugo
– Shirika la Viwango
21
www.tfda.or.tz
Ahsanteni Sana
22
www.tfda.or.tz