Ebola Ebola, awali ilijulikana kama homa ya hemojari ya Ebola, ni ugonjwa kali, kila mara hatari kwa binadamu na jamii ya nyani (kama vile nyani, gorila, na sokwe). Ebola ni ugonjwa nadra na hatari unaosababishwa kwa kuambukizwa virusi vinavyopatikana kwenye familia ya Filoviridae, jeni ya Ebolavirus. Kuna spishi tano zilizotambuliwa za Ebolavirus, nne ambazo zimesababisha ugonjwa kwa binadamu: ebolavirus ya Zaire; ebolavirus ya Sudan; ebolavirus ya Tai Forest , awali ebolavirus ya Kodivaa ; na ebolavirus ya Bundibugyo. Ya tano, ebolavirus ya Reston , imesababisha ugonjwa katika familia ya nyani lakini sio kwa binadamu. Ebola inapatikana katika nchi kadhaa barani Afrika. Spishi ya kwanza ya Ebola iligunduliwa mwaka wa 1976 karibu na Mto Ebola ambao unafahamika sasa kama Jamuhuri ya Kidemokorasia ya Kongo. Tangu wakati huo, mikurupuko imeonekana kujitokeza mara kwa mara barani Afrika. Hodhi jeshi asili ya Ebola inasalia kutojulikana. Hata hivyo, kwa msingi wa ushahidi unaopatikana na asili ya virusi sawa, watafiti wanaamini kuwa virusi vinatokana na wanyama huku popo wakiwa na uwezekano zaidi wa kuwa hodhi. Nne kati ya aina ndogo tano hutokea katika mnyama jeshi asili katika Afrika. Maambukizi Kwa sababu bado hodhi jeshi asili ya Ebola haijatambuliwa, namna ambavyo virusi huonekana kwanza kwa binadamu mwanzoni mwa mkurupuko haijulikani. Hata hivyo, watafiti wanaamini kuwa mgonjwa wa kwanza huambukizwa kupitia mgusano na mnyama aliyeambukizwa. Wakati ambapo maambukizo yanatokea kwa binadamu, kuna njia nyingi ambazo virusi vinaweza kusambazwa kwa wengine. Zinajumuisha: • mgusano wa moja kwa moja na damu au maji maji ya mwili (pamoja na lakini sio tu kinyesi, mate, mkojo, matapishi na manii) ya mtu anayeugua Ebola. • mgusano na vifaa (kama sindano, na sirinji) ambavyo vimesibikwa kwa damu au maji maji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa au wanyama walioambukizwa Visuri vilivyo kwenye damu au maji maji ya mwili vinaweza kuingia kwenye mwili wa mtu mwengine kupitia ngozi iliyopasuka au kiwamboute kisicholindwa, kwa mfano, macho, pua, au kinywa. Kila mara visuri vinavyosababisha Ebola husambaa miongoni mwa familia na marafiki, kwa sababu wanagusana kwa karibu na damu au maji maji ya mwili wanapotunza watu wanaougua. Wakati wa mikurupuko ya Ebola, ugonjwa unaweza kuenea haraka kwenye mipangilio ya kituo cha afya, kama vile kliniki na hospitali. Mfinduo wa Ebola unaweza kutokea katika mipangilio ya kituo cha afya ambapo wafanya kazi wa hospitali hawavai mavazi ya kujikinga yanayostahili pamoja na barakoa, gauni, glovu, na mavazi ya kukinga macho. Vifaa maalum vya matibabu (vinavyopendelewa kutupwa, ikiwezeskana) vinafaa kutumiwa na mfanya kazi wa kituo cha afya anayetoa huduma ya utunzaji kwa mtu anayeugua Ebola. Usafishaji na utupaji unaofaa wa vifaa, kama vile sindano na sirinji, pia ni muhimu. Iwapo vifaa haviwezi kutupwa, lazima visafishwe kabla ya kutumiwa tena. Bila usafishaji wa kutosha wa kifaa, maambukizi ya virusi yanaweza kuendelea na kuongeza mkurupuko. Ishara na Dalili Mtu aliyeambukizwa Ebola hana hatari ya kueneza hadi dalili zitokee. Ishara na Dalili za Ebola kwa kawaida zinajumuisha: • • • • Homa (zaidi ya 38.6°C au 101.5°F) Maumivu makali ya kuumwa na kichwa Maumivu ya misuli Kutapika Kituo cha Taifa kwa Magonjwa ya Kuambukizwa Yanayojitokeza na Kuzambazwa Miongoni mwa Wanyama Divisheni ya Pathojeni na Patholojia (DHCPP) yenye Madhara Makuu • • • Kuendesha Maumivu ya tumbo Kutoka damu au kuvilia kusikoweza kufafanuliwa Huenda dalili zikatokea mahali popote kutoka siku ya 2 had 21 baada ya mfiduo wa Ebola lakini uwastani wa siku 8 hadi 10. Kupata nafuu kutokana na Ebola kunategemea mfumo wa kingamaradhi wa mgonjwa. Watu wanaopata nafuu kutokana na maambukizo ya Ebola wanakua na kingamwili zinazochukua muda wa angalau miaka 10. Hatari ya Mfiduo Ebola inapatikana katika nchi kadhaa barani Afrika. Tangu mwaka wa 1976, mikurupuko ya Ebola imetokea katika nchi zifuatazo: • • • • • • • Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Gaboni Sudan Kusini Kodivaa Uganda Jamuhuri ya Kongo (ROC) Afrika Kusini (ililetwa) • • • • • Gine Liberia Siera Leoni Senegali Nijeria Kwa sababu hodhi jeshi asili ya Ebola, na namna ambavyo usambazaji wa virusi kwa binadamu husalia kutojulikana, kutathmini hatari katika maeneo ambayo unapatikana ni vigumu. Wakati wa mikurupuko ya Ebola, walio na hatari kubwa ni pamoja na wafanya kazi wa kituo cha afya na familia na marafiki za watu walioambukizwa Ebola. Wafanya kazi wa kituo cha afya barani Afrika wanafaa kupata ushauri kutoka Udhibiti wa Maambukizo kwa Homa za Virusi vya Hemoraji Katika Mpangilio wa Huduma ya Afya ya Kiafrika ili kujifunza jinsi ya kudhibiti mipangilio hii. Wataalam wa matibabu nchini Marekani wanafaa kupata ushauri kutokaUzuiaji wa Maambukizo na Mapendekezo ya Udhibiti kwa Wagonjwa Walio Hospitalini Wanaojulikana au Kushukiwa kuwa na Homa ya Hemojari ya Ebola katika Hospitali za Marekani. Ubainishaji wa ugonjwa Ubainishaji wa ugonjwa wa Ebola kwa mtu aliyeambukizwa kwa siku chache tu ni vigumu kwa sababu dalili za mapema, kama vile homa, sio bainifu kwa maambukizo ya Ebola na zinaonekana kila mara kwa wagonjwa walio na maradhi yanayotokea kwa kawaida, kama vile malaria na homa ya matumbo. Hata hivyo, iwapo mtu ana dalili za Ebola na amegusana na damu au maji maji ya mwili wa mtu anayeugua Ebola, mgusano na vifaa ambavyo vimesibikwa kwa damu au maji maji ya mwili wa mtu anayeugua Ebola au mgusano na wanyama walioambukizwa, mgonjwa anafaa kutengwa na wataalam wa afya ya umma kuarifiwa. Kisha sampuli kutoka kwa mgonjwa zinakusanywa na kujaribiwa ili kuthibitisha maambukizo. Majaribio ya maabara yanayotumiwa katika ubainishaji wa ugonjwa ni pamoja na Muda wa Maambukizo Baada ya siku chache dalili huanza Majaribio yanayopatikana ya ubainishaji wa ugonjwa - Jaribio la Antigen-capture enzyme-linked immunosorbent assay (ELISA) - IgM ELISA - Mjibizo wa msururu wa Polymerase (PCR) - Kutengwa kwa virusi Baadaye wakati wa ugonjwa au baada ya kupata nafuu - Kingamwili za IgM na IgG Yanayojiri baada ya wagonjwa walioaga - Jaribio la Immunohistochemistry - PCR - Kutengwa kwa virusi Matibabu Kwa sasa hakuna chanjo au dawa bainifu (kama vile dawa za kukinga virusi) zilizothibitishwa kuwa na ufanisi dhini ya Ebola. Dalili za Ebola zinatibiwa pindi zinavyoonekana. Hatua msingi zifuatazo, zikitumiwa mapema, zinaweza kuboresha pakubwa nafasi ya kuishi: o Kutoa maji maji ya kupitia kwenye sindano (IV) na kusawazisha elekroliti (chumvi ya mwili) o Kudumisha hali ya oksijeni na shinikizo la damu o Kutibu maambukizi mengine iwapo yatatokea Matibabu ya muda ya Ebola ni muhimu lakini yana changamoto kwa kuwa ugonjwa ni mgumu kubainishwa kwenye kliniki katika awamu za mapema za maambukizo. Kwa sababu dalili kama vile maumivu ya kichwa au homa hazibainiki kwa Ebolaviruses, huenda kesi za Ebola zinaweza kutobainishwa vilivyo mapema. Hata hivyo, iwapo mtu ana dalili za Ebola na amegusana na damu au maji maji ya mwili wa mtu anayeugua Ebola, mgusano na vifaa ambavyo vimesibikwa kwa damu au maji maji ya mwili wa mtu anayeugua Ebola, au mgusano na wanyama walioambukizwa, mgonjwa anafaa kutengwa na wataalam wa afya ya umma kuarifiwa. Matibabu yanayosaidia yanaweza kuendelea kwa mavazi ya kinga yanayostahili hadi sampuli kutoka kwa mgonjwa zijaribiwe ili kuthibitisha maambukizo. Matibabu ya majaribio yamejaribiwa na kuthibitishwa kuwa na ufanisi kwenye baadhi ya wanyama lakini bado hayajatathminiwa kwa binadamu. Kuzuia Wakati kesi za ugonjwa hutokea, kuna ongezeko la hatari ya ueneaji katika mipangilio ya kituo cha afya. Kwa hivyo, lazima wafanya kazi wa kituo cha afya waweze kutambua kesi ya Ebola na kuwa tayari kutumia hatua za kudhibiti maambukizo. Lengo la mbinu hizi ni kuzuia mgusano na damu au maji maji ya mwili ya mgonjwa aliyeambukizwa. Utaratibu unaostahili unajumuisha: o kutengwa kwa wagonjwa wa Ebola kutokana na kugusana na watu wasio na kinga o kuvaa mavazi yenye kinga (pamoja na barakoa, glovu. gauni zisizopenyeka, na miwani au ngao za uso) na watu waotunza wagonjwa wa Ebola o matumizi ya hatua nyingine za kuzuia maambukizo (kama vile usafishaji kamili wa kifaa na matumizi ya kila mara wa kiua viini) o Epuka kugusa mili ya wagonjwa walioaga dunia kutokana na Ebola Wafanya kazi wa kituo cha afya pia wanafaa kuwa na uwezo wa kuomba majaribio ya ubainishaji au kuandaa sampuli kwa kusafirisha na kujaribia kwingine. CDC, kwa ushirikiano na Shirika la Afya Ulimwenguni, imekuza seti ya miongozo kusaidia kuzuia na kudhibiti usambazaji wa Ebola. Udhibiti wa Haki ya Maambukizo kwa Homa za Virusi vya Hemoraji Kwenye Mpangilio wa Afya ya Afrika, kijitabu huelezea jinsi ya: o tambua kesi za homa ya virusi vya hemoraji o zuia maambukizo zaidi katika mpangilio wa huduma ya utunzaji wa afya kwa kutumia nyenzo zinazopatikana na rasilimali chache za fedha
© Copyright 2026 Paperzz